Mechi ya kukata na mundu iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu
kati ya mashabiki wa Yanga dhidi ya wale wa Simba, wote wanafunzi wa Chuo Kikuu
cha Tumaini mjini Arusha imemalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mechi iliyopigwa leo jioni na kupewa jina la NANI MTANI JEMBE MAKUMIRA ilikuwa kali nay a kuvutia huku mashabiki wa kila upande wakitambiana.
![]() |
| KIKOSI CHA SIMBA BILA YA LOGARUSIC |
![]() |
| KIKOSI KAMILI CHA YANGA BILA VAN DER PLUIJM |
Pamoja na timu zote kuanza mchezo kwa kujiamini huku
zikionyesha zimepania kupata ushindi, Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kuonyesha
wao ni watani jembe baada ya kupata bao katika dakika ya 25, kwa ‘mpira
uliokufa’ kupitia kwa Rodrick John.
Kila upande ulishambulia, Yanga wakitaka kuongeza na Simba
wakitaka kusawazisha, lakini ‘milango’ ikawa migumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko kadhaa na
kushambuliaji kwa zamu, ufundi, mbwembwe, kasi, vyenga vikitawala, lakini bado
mambo yalikuwa magumu kwa Simba kupata bao.
Huku wengi wakiamini, Yanga watakuwa wamelipa kile kisasi
cha Yanga ya “ukweliukweli” kulala kwa mabao 3-1, dhidi ya Simba ya “ukweliukweli”
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar Desemba 21, mwaka jana, mambo yakabadilika.
Kwani Simba walionyesha kuwa ni wafalme wa pori na
wasiokata tamaa wanaposaka nyama baada ya Joshua Ibunga kuisawazishia katika
dakika ya 81. Bao hilo lilifungwa baada ya Simba kusukuma shambulizi
lilosababisha piga nikubutue kwenye lango la Jangwani ambao walishindwa kuwazuia
Msimbazi kusawazisha.
kwa free kick kali
ktk dk ya 25 kipind cha kwanza. Simba walisawazisha kipind cha pili dk ya 81
baada ya kutokea piga nikupige golini kwa yanga, mfungaji wa goli hilo ni
Joshua Ibunga.
Mgeni wa nguvu au heshima katika mechi hiyo alikuwa Rais au
Prezidaa wa Serikali ya Wanachuo, Mheshimiwa John ambaye hata hivyo haikuelezwa
anashangilia upande upi, njano na kijani au redi na waiti.
![]() |
| MASHABIKI WA MSIMBAZI |
![]() |
| WATU WA JANGWANI |




.jpg)








0 COMMENTS:
Post a Comment