Kocha Mkuu wa Azam FC, Joseph Omog,
amesema anahitaji mechi mbili za kirafiki kujipima kabla ya kuanza mzunguko wa
pili wa Ligi Kuu Bara ili kukiimarisha kikosi chake.
Azam iliondolewa katika michuano ya
Kombe la Mapinduzi kwa kuvuliwa ubingwa waliokuwa nao ambapo wameanza mazoezi
jana Jumanne, tayari kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu unaoanza kutimua vumbi
Januari 25.
Katibu Mkuu wa Azam FC, Idrissa Nassor, alisema wapo katika mchakato wa kusaka
timu mbili ili kucheza michezo ya
kirafiki kabla ya kuanza ligi kutokana na mahitaji ya kocha Omog.
“Kocha anahitaji mechi mbili za kirafiki
tuweze kumtafutia kabla ya kuanza mzunguko wa pili wa ligi na kwa sasa tupo
katika mchakato huo ili kupata timu zenye ubora wa kuweza kujipima nazo.
“Timu tunazosaka ni za hapahapa nchini
na siyo nje ya nchi, mechi hizo zitamsaidia kocha kuweza kukiandaa kikosi chake
kabla mzunguko wa pili haujaanza.
“Kuhusu kupokonywa ubingwa, hilo halina
shida kwetu kwani tumekuwa tukilimiliki kombe kwa miaka miwili mfululizo, hivyo
kuna klabu nyingine zilikuwa zikihitaji na sisi tutajipanga kwa mambo mengine
na tunasubiria mwakani,” alisema Nassor.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment