Wakati Yanga inashuka leo
dimani kucheza mechi ya kirafiki, Kocha Hans van Der Pluijm amewataka wachezaji
wake wauchezee mpira.
Msemaji wa Yanga, Baraka
Kizuguto amesema kocha huyo mpya amewataka wachezaji kuuchezea zaidi mpira.
“Amewataka kujiamini na
kuuchezea mpira lakini kwa malengo. Kocha ameonekana kuwaamini wachezaji.
“Kikosi kimefurahisha,
hivyo anachotaka ni wao kujiamini na kuuchezea mpira.
“Tayari ameanza mazoezi na
ukweli wachezaji wanaonekana kuyakubali na ukumbuke walianza vizuri na mazoezi
pia mazuri kutoka kwa Kocha Mkwasa,” alisema.
Yanga iko kambini Uturuki
kwa wiki mbili na tayari imecheza mechi mbili za kirafiki na kushinda zote.








0 COMMENTS:
Post a Comment