![]() |
| LOGARUSIC AKIWAFUNDISHA JAMBO WAANDISHI WA CHAMPIONI |
Pamoja na kwamba leo
watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba wanataka mechi moja ya
kirafiki.
Kocha Mkuu wa Simba,
Zdravko Logarusic ametaka kupata mechi moja ya kirafiki ya kimataifa.
“Kocha amesema anataka
mechi moja ya kirafiki ya kimataifa baada ya kucheza na Mtibwa Sugar.
“Baada ya hapo, atakuwa
katika nafasi ya kuangalia vizuri afanye nini na kikosi chake na sisi
tunalifanyia kazi,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Simba, Swed
Nkwabi.
Simba ilifanikiwa kuingia
fainali ya Kombe la Mapinduzi ambalo walilipoteza kwa KCC ya Uganda kwa
kufungwa bao 1-0.








0 COMMENTS:
Post a Comment