Baada ya Kocha wa Simba, Zdravko
Logarusic kutua Uwanja wa Taifa jijini Dar, jana kuishuhudia Yanga ikicheza na
Ashanti United, leo wa Yanga naye amejibu mapigo.
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm
naye ametua uwanjani hapo na kuishuhudia Simba ikivaana na Rhino ya Tabora na
kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Pluijm alitua uwanjani hapo akiwa na
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ambaye alikuwa akimpa mambo kadhaa aliyotaka
kujua kuhusiana na kikosi cha watani wake hao Simba.
Kocha huyo raia wa Uholanzi, hiyo ilikuwa
mara yake ya pili kuingia Taifa baada ya jana kuingia kwa mara ya kwanza na
kuingoza Yanga kuishinda kwa mabao 2-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment