Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi,
amesema siri ya ushindi kwenye mechi yao dhidi ya Kagera Sugar ni kujituma kwa
wachezaji wake pamoja na kufuata maelekezo yake.
Mbeya City ambayo inaendelea kuzitesa
timu za Ligi Kuu Bara, juzi Jumamosi iliifunga Kagera Sugar bao 1-0 ugenini
kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera na kuzidi kuwapumulia vinara Yanga kwa
tofauti ya pointi moja.
Mwambusi amesema baada ya kutoka kwenye michuano ya Mapinduzi ambayo kikosi
chake hakikufanya vizuri, aliwapanga upya vijana wake na kuanza maandalizi kwa
kuufanyia kazi upungufu uliojitokeza kwenye michuano hiyo.
Alisema pia anawapongeza mabeki wa timu
zote kwa kuwa walifanya kazi ya ziada kuwazuia washambuliaji wa timu zote
lakini zaidi wa Mbeya city ambao wanaonekana kuimarika.
Aliongeza kuwa mechi yao dhidi ya Ruvu
itakayochezwa keshokutwa Jumatano, itakuwa ngumu na matokeo yatapatikana ndani
ya dakika 90.
“Siri ya ushindi ni maandalizi mazuri,
pia Kagera walikuwa vizuri lakini zaidi pongezi kwa mabeki wa timu zote kwa
kuwa walifanya sana kazi ya kuzuia.
“Mechi yetu na Ruvu siwezi kusema
tutashinda au la, tambua mimi naheshimu timu zote, kwa hiyo matokeo ni dakika
90 na nitayapokea yoyote,” alisema Mwambusi.
0 COMMENTS:
Post a Comment