VAN DER PLUIJM NA MSAIDIZI WAKE MKWASA, LEO. |
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm
amesema upepo mkali na uwanja mbovu wa Mkwakwani ni chanzo cha wao kushindwa
kufanya vizuri.
Van Der Pluijm amesema walishindwa
kuweka mpira chini kama walivyotarajia kutokana na uwanja kutokuwa katika hali
nzuri kwenye upande wa kuchezea.
Lakini bado akasisitiza, walipojaribu
kuinua mipira juu, haikuwa ikienda kwa kasi inayotakiwa kutokana na kuwa na
upepo mkali.
“Niliwaambia wachezaji kuongeza umakini
kwa kuwa upepo pia ulitusumbua na kusababisha mpira kupoteza uelekeo,” alisema van
Der Pluijm.
“Bado tuna nafasi ya kujirekebisha,
tunaweza tukafanya vizuri zaidi ya hapo, lakini lazima tujipange na kitu kizuri
tumepata pointi moja.”
Yanga imeshuka kileleni baada ya
kuzidiwa pointi moja na Azam FC yenye 33 sasa baada ya kuishinda Rhino 1-0 na
Yanga inabaki na 32 kutokana na sare hiyo ya Mkwakwani.
0 COMMENTS:
Post a Comment