Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen,
amesema alimpigia kura ya Mchezaji Bora wa Dunia, kiungo wa Bayern Munich,
Franck Ribery.
Cristiano Ronaldo alitwaa Tuzo ya Mwanasoka
Bora wa Dunia wa mwaka jana juzi usiku zilipotangazwa kwenye makao makuu ya
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Zurich, Uswis.
Kim amisema kura yake ilikwenda kwa
mchezaji huyo kutokana na kuamini ni bora kwa sababu kiwango chake si cha
kubeza lakini kura nyingi ziliweza kuangukia kwa Ronaldo.
Kim alisema kuwa Messi na Ronaldo si
wachezaji wa kuwabeza kutokana na viwango vyao na wamekuwa wakizisaidia sana
timu zao lakini kwake Ribery alikuwa zaidi.
“Niliweza kumpatia kura yangu Franck
Ribery kwa sababu niliamini angeweza kupata
nafasi ya kuwa mwanasoka bora kutokana na uwezo
wake na kipaji chake alichokionyesha katika timu alizopitia na alipo
sasa.
“Lakini si kwamba Ronaldo hakustahili,
hapana, lakini kwa upande wangu Ribery alikuwa zaidi,” alisema Kim.
Ribery ameshika nafasi ya tatu baada ya
Lionel Messi wa Barcelona kushika ya pili nyuma ya Cristiano Ronaldo.
0 COMMENTS:
Post a Comment