January 18, 2014



Mtibwa Sugar imefunga Simba bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.


Pamoja na kipigo hicho, Kocha wa Simba, Dravko Logarusic amesema wako kwenye mchakato wa kusaka kikosi, hivyo hawana sababu ya hofu.
“Hakuna sababu ya kuwa na hofu, najua kufungwa si kitu kizuri lakini ni kitu kizuri kwetu kwa kuwa tunajiandaa na ligi.
“Hivyo tunajaribu kufanya kila linalowezekana ili kuwa na kikosi bora kabisa, kufungwa kunatuumiza lakini tukutumie kama njia sahihi ya kujifunza,” alisema Logarusic.

Katika mechi hiyo kocha huyo raia wa Croatia, alifanya mabadiliko ya wachezaji wote walioanza katika kikosi cha kwanza isipokuwa beki Kaze.

Mechi ilikuwa na ushindani wa juu na Mtibwa Sugar ndiyo walioonyesha kiwango kizuri zaidi hasa kipindi cha pili.

Huu ni mchezo wa pili mfululizo Logarusic kufungwa, mara ya mwisho Simba ililala bao 1-0 katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya KCC ya Uganda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic