Kocha Mkuu wa JKT Oljoro ya Arusha,
Hemed Morocco, amesema ameshangazwa kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Coastal
Union ya jijini Tanga kwa kuwa timu yake ilistahili kushinda kutokana na
kiwango ilichokionyesha.
Coastal walilazimishwa sare hiyo juzi katika
mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani,
Tanga.
Morocco, aliyekuwa kocha mkuu wa Coastal katika mzunguko wa kwanza kabla ya
kutimuliwa, alisema katika mchezo huo wa juzi, walikuwa na uwezo wa kuwafunga
wapinzani wao hao kwenye uwanja wao wa nyumbani.
“Yaani inashangaza kwa kweli kutoka sare
na Coastal kutokana na kiwango tulichokionyesha, tulicheza mpira mzuri zaidi
yao na tulikuwa tukifanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwao, ila
nafikiri haikuwa bahati yetu kwa sababu tuliwakamata kwa kiwango kikubwa,”
alisema Morocco.
0 COMMENTS:
Post a Comment