Ilikuwa vigumu sana kukubaliana na
rafiki na wasomaji wengi wa makala zangu waliokuwa wakinishawishi kuanzisha
blog.
Lakini wengi walizidi kunishawishi na
mwisho nikaona nifanye hivyo. Sina maana sikuwa na uwezo wa kufanya hivyo,
lakini nia ya ushindani ilikuwa inanitatiza.
Ninapoanzisha kitu napenda kiongoze,
kiwe cha kwanza lakini niliona sikuwa na muda wa kutosha kwa ajili ya
kuisimamia vizuri blog yangu.
Sikupenda kuwa msindikizaji au kufanya
kwa kubahatisha, lakini niliamua kuingia angalau kwa 50% na nimekuwa
nikiendelea kujiongeza.
Muda ni mchache kwa kuwa ni mwajiriwa,
pia ninasimamia miradi yangu, lakini bado najitahidi kuhakikisha ifikie siku
blogu hii isimame ninavyotaka na kukidhi kiu cha wengi.
Tathmini yangu inanionyesha bado, sasa
ndiyo takribani mwaka lakini nimepata wasomaji zaidi ya milioni 2. Kwangu naona
hili ni deni na rekodi nzuri kabisa.
Shukurani kwenu kwa kuniunga mkono mwaka
2013, mmeonyesha mnaniamini name nashukuru kwa upendo wenu na imani yenu
kwangu.
Kweli ninabanwa kutokana na ajira ambayo
inaendana na ushindani mkubwa, kwani kila mmoja sasa anataka kufanya zaidi ya
ninachofanya.
Nimezalisha idadi kubwa ya waandishi
wanaotaka kufanikiwa, wako wanaonitaja na wasiokubali hilo hadharani, lakini
ndani ya nafsi zao wanaweza kulisikia hilo, kwamba wanafanya hivyo kutokana na
walichokiona kwangu.
Nirudie ninawashukuru sana kwa kuniunga
mkono mwaka 2013, wasomaji, rafiki, jamaa na ndugu zangu. Wote nawashukuru sana.
Familia yangu, timu ya gazeti la
Championi pia kwa sapoti lakini niwaombe tuwe pamoja mwaka 2014 ili tuendelee
kupamba.
Shukurani nyingine ziende moja kwa moja kwa wadhamini wa blog ya SALEHJEMBE, wao wanachangia mambo kadhaa na ni changamoto kwangu.
Idadi ya wasomaji niliyoipata kwa
kipindi cha miezi 10 ni kubwa mno na ninastahili kuwashukuru na kujivunia.
Malengo ni kuifikia zaidi ya mara tatu
kwa 2014l, nawahakikishia ninaweza na ninajiamini nitafanya hivyo kwa kuongeza
juhudi na kutenga muda zaidi angalau kwa ahili ya blogu.
Hakika si kazi lahisi lakini
nitajitahidi kwa kuwa nataka kutimiza malengo.
Nawashukuru na ninawaomba muendelee
kuniunga mkono mwaka 2014.
Nawaombea afya njema kwa mwaka 2014,
ninaamini afya ndiyio mtaji mkubwa kwa mwanadamu yoyote kuliko kitu kingine.
Mwenyezi Mungu anatupenda, tumshukuru
kwa pamoja na kumuomba atujaalie kheri katika mwaka wa 2014.
NAWAPENDA WOTE.
kazi nzuri umeifanya kwa kweli na toka unaanza na hii blog nlikuandikia ujumbe facebook wa kukutia nguvu na kukomaa nayo na ukanijibu utapambana, kwa kweli blog yako ni ya kipekee tofauti na blogs nying za kibingo za michezo.
ReplyDeletebinafsi naitembelea blog hii mara kwa mara hata mara tatu kwa siku. hongera sana na kaza buti mkuu wangu
Ni kweli upo tofauti sana na blogs nyingi ambazo waandishi wake wamejaa tabia za ushabiki pasipo kuzingatia ukweli. Haiwezekani kila siku wewe ni kukosoa timu hiyohiyo kila siku na kuwa haina mazuri. Nawashauri hao wenzio wajifunze kwako kwani unachambua, unakosoa penye kustahili na kusifia penye haki ya kufanyiwa hivyo. Umekataa kutumiwa kama akina Fulani. HONGERA.
ReplyDelete