Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm
ameamua ‘kumlipa’ yule wa Simba, Zrdavko Logarusic kwa kwenda uwanja wa Taifa,
leo.
Logarusic, jana aliibuka uwanjani na
kuishuhudia Yanga ikicheza dhidi ya Ashanti United na kuibuka na ushindi wa
mabao 2-1 kwa taabu.
Leo, van Der Pluijm, raia wa Uholanzi
ataingia uwanjani hapo kushuhudia mechi kati ya Simba dhidi ya Rhino ya Tabora
utakaochezwa Taifa.
“Kweli kocha anakwenda Taifa, anataka
kuiona Simba,” kilieleza chanzo cha uhakika.
0 COMMENTS:
Post a Comment