Mshambuliaji nyota wa Atlético Madrid, Diego
Costa sasa ameingia kwenye za wachezaji wengine wakubwa kama Lionel Messi, Gareth
Bale na Luis Suárez.
Kampuni ya vifaa ya Adidas ambayo
imeingia naye mkataba, itaanza kumtengenezea viatu maalum kwa ajili yake kama
ambavyo hufanya kwa nyota hao.
Mshambuliaji huyo mwenye asili ya
Brazil ambaye sasa ana uraia wa Hispania amekuwa tishio kwenye Ligi ya Hispania
‘La Liga’ kutokana na kasi yake ya upachikaji mabao inayowapa hofu wakali kama
Messi na Cristiano Ronaldo.
0 COMMENTS:
Post a Comment