Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred
Felix Minziro, amesema ikiwa timu yake hiyo isipokuwa makini katika michezo ya
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, inaweza kupoteza ubingwa.
Minziro alitupiwa virago na Yanga hivi
karibuni kufuatia madai ya kutofanya vizuri kwa benchi lote la ufundi. Yanga
imeshaporomoka mpaka nafasi ya pili (kabla ya jana) kutokana na kutoka suluhu
na Coastal Union.
Minziro amesema matokeo ya Yanga si mabaya sana, wala si mazuri sana, lakini
wachezaji wanahitaji kubadilika kwa kukaza buti ili waweze kufanikiwa kutetea
ubingwa wao.
“Wachezaji wanahitaji kucheza kitimu
zaidi kwa kuhakikisha wanajituma, ligi ni ngumu kutokana na kila timu kujipanga
kuhakikisha inashinda katika michezo yake,” alisema Minziro.
0 COMMENTS:
Post a Comment