February 7, 2014



 
CHEKA AKIWA NA SALEH ALLY
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka ‘amemvaa’ Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic kwa kumshauri kuiimarisha safu ya kiungo na ushambuliaji ya timu hiyo ili timu iweze kufanya vizuri zaidi katika michezo yake.


Akizungumza na SALEHJEMBE baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, mjini hapa, Cheka ambaye ni shabiki wa Simba, alisema timu yake ina matatizo katika safu ya kiungo na ushambuliaji.

“Sijui michezo mingine, lakini katika mchezo wa leo (Jumatano) timu haikuchezesha vizuri katikati na mbele, mwalimu anapaswa kuliangalia hili,” alisema Cheka ambaye pia alikuwepo Uwanja wa Taifa, wikiendi iliyopita katika mechi ya Simba dhidi ya JKT Oljoro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic