Shirikisho la Soka la Kimataifa
(Fifa) limeruhusu mshambuliaji Emmanuel Okwi kuichezea Yanga.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya
TFF ambazo zimethibistishwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Mwesigwa
Celestine zimesema kuwa Okwi sasa ni huru.
“Kweli hilo tumetaarifiwa lakini
tutalizungumzia baadaye,” alisema.
TFF ndiyo ilisimamisha usajili wa
Okwi kwa madai ya kutaka ufafanuzi kutokana na kesi tatu za kimsingi kati ya
Okwi, Etoile du Sahel.
Sasa Okwi atakuwa huru kuanza
kuitumikia Yanga ambayo imesamjili kwa dau la zaidi ya dola 100,000 (Sh milioni
160).








0 COMMENTS:
Post a Comment