Kocha Hans van Der Pluijm amesema
amefurahishwa na kiwango cha kiungo wake Athumani Idd ‘Chuji’.
“Ni kati ya wachezaji wazuri, atakuwa
msaada,” alisema kocha huyo Mholanzi huku akisisitiza wachezaji wake wamekuwa
wakijituma na anategemea makubwa.
Yanga iko kambini Bagamoyo kujiandaa
kucheza na Wacomoro katika mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Chuji hakuwa amewahi kufanya kazi na van
Der Pluijm kabla kwa kuwa hakwenda Uturuki kutokana na kusimamishwa kwa utovu
wa nidhamu.
0 COMMENTS:
Post a Comment