CHANGA (WA TATU KUSHOTO MSITARI WA NYUMA) WAKATI AKIKIPIGA JKT RUVU |
Bado tetesi zinaendelea kugubika kifo
cha mshambuliaji nyota wa zamani wa Yanga, Omary Changa ambaye ameuwawa.
Mwili wa Changa uliokotwa hivi karibuni
katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam na haikujulikana nini kilitokea.
Lakini taarifa zinaeleza amenyongwa na
nyingine zinaeleza amepata kipigo kutoka kwa watu wasiojulikana.
“Lakini tumeambiwa kuwa uchunguzi wa
madaktari unaonyesha alishambuliwa ikiwa ni pamoja na kupigwa na kitu kizito
usoni.
“Ila kila kitu kuhusiana na hilo
tutapata leo na baada ya hapo tunaweza kufuatilia,” alisema ndugu yake wa
karibu.
Changa aliwahi kucheza katika timu
kadhaa zikiwemo JKT Ruvu, Moro United na Kagera Sugar na alikuwa kati ya
mastraika noma.
0 COMMENTS:
Post a Comment