Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama cha Soka Zanzibar
(ZFA) kisiwani Pemba, kimemfungia kwa muda wa mwaka mmoja shabiki maarufu
kisiwani hapa, Simai Abdallah Simai ‘Sakala’, kuingia Uwanja wa Gombani
kuangalia mechi.
Sakala amekumbwa na rungu
hilo kali kutoka kwa chama hicho kutokana na kudaiwa kuzidisha lugha kali muda
wote anapokuwa uwanjani.
Barua ya chama hicho ina
kumbukumbu namba REF.NO.ZFA/T/BAF/VO.V/P/123, ya Februari 2, 2014 kwenda kwa
Simai Abdalla Simai, 151 KJ Vitongoji.
Barua hiyo imesema Sakala
amekuwa akisababisha usumbufu mkubwa uwanjani hapo, wakati wa michezo na
kuondoa nidhamu ya michezo kisiwani, jambo ambalo halikubaliki.
Aidha, barua hiyo imesema
kuwa, adhabu hiyo inaanza tarehe ya kutolewa mpaka kumalizika kwa msimu huu wa
ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment