Kocha Mkuu wa Ashanti United, Abdallah Kibadeni amesema hawezi kukaa
na timu inayofungwa mara kwa mara na kuamua kuweka wazi kuwa ikitokea timu yake
ikafungwa mechi tatu mfululizo, basi atatangaza kujiuzulu.
Kibadeni alitoa kauli hiyo baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu, katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Chamazi,
ambapo mfungaji alikuwa Iddi Selemani.
Kibadeni alisema: “Kufungwa mechi
tatu mfululizo ni bora nijiuzulu kwa kuwa timu itakuwa imenishinda, lakini
katika mchezo wa leo (juzi) vijana wamecheza vizuri, ila tulitakiwa kufunga
mabao mengi zaidi.”
Kabla ya mechi ya jana, Ashanti ilikuwa imefungwa mechi mbili
mfululizo. Upande wa Kocha wa JKT Ruvu, Mbwana Makata, alitupia lawama kwa
waamuzi wa mchezo huo na kusema ndiyo waliyoinyima timu yake ushindi.
0 COMMENTS:
Post a Comment