Beki ‘kisiki’ wa Ruvu Shooting, Michael
George, huenda akarejea uwanjani mapema badala ya miezi mitatu kama
ilivyoripotiwa awali, kufuatia afya yake kuimarika haraka.
Beki huyo aliyejizolea umaarufu kwa
kuwadhibiti mastraika wa Simba na Yanga katika raundi ya kwanza ya Ligi Kuu
Bara, yupo nje akiuguza jeraha la mguu wa kulia uliovunjika katika mazoezi ya
timu yake kujiandaa na mzunguko wa pili, siku chache kabla ya pazia
kufunguliwa.
Msemaji wa Ruvu, Masau Bwire, amesema tayari
nyota huyo amefunguliwa bandeji ngumu (P.O.P). “Taarifa za daktari na anavyoonekana,
hatakaa nje miezi mitatu kama ilivyosemekana awali,” alisema Bwire.
0 COMMENTS:
Post a Comment