February 7, 2014


MACHAKU WAKATI AKIKIPIGA SIMBA


Kasheshe kubwa lilizuka juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar kulipokuwa na mechi baina ya JKT Ruvu na Ashanti United baada ya mshambuliaji wa JKT, Salum Machaku kuamua kumvamia shabiki jukwaani.


Katika mechi hiyo ambayo Ashanti iliibuka na ushindi wa bao 1-0, kulikuwa na tambo nyingi kwa mashabiki waliojitokeza kuangalia mchezo huo, kitu kilichoelezwa kuchochea ugomvi huo.

Shabiki mmoja uwanjani hapo anayedhaniwa kuwa ni wa Ashanti, alimzomea Machaku na kumtupia maneno ya dhihaka wakati alipokuwa akielekea benchi, baada ya kutolewa na kocha wa timu hiyo, Mbwana Makata dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza.

Hata alipokaa kwenye benchi, bado shabiki huyo aliendelea kumshambulia vikali kwa maneno, Machaku akashindwa kuvumilia na kuamua kunyanyuka na kumfuata juu kwenye jukwaa alilokuwepo shabiki huyo na ndipo vurugu zilipoanza.

Wakiwa kwenye mtifuano mkubwa wa kila mmoja kutaka kumchapa mwenzake, ndipo mchezaji mmoja wa JKT na kocha wa timu B ya Ashanti, Maalim Saleh ‘Romario’ walipotokea na kuwagombelezea.

Baada ya muda Machaku alitulia na shabiki pia kutulizwa na wenzake ndipo hali iliporudi kuwa shwari kama awali na mpira kuendelea kwa amani.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic