MUSLAH AKIWA UWANJANI LEO DAKIKA CHACHE KABLA YA KUANZA KWA MECHI KATI YA LIVERPOOL DHIDI YA ARSENAL ILIYOMALIZIKA KWA WENYEJI KUSHINDA KWA MABAO 5-1. |
Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya klabu ya
Simba, Muslah Al Rawah leo alikuwa uwanjani akishuhudia live Liverpool
ikiibanjua Arsenal 5-1.
Al Rawah ambaye hivi karibuni
alimzawadia kiungo nyota wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’, alikuwa uwanjani
Anfield jijini Liverpool ikiitandika Arsenal mabao hayo matano.
“Nimeshuhudia mechi na ilikuwa faraja
kwangu kwa kuwa ni sahabiki wa Liverpool,” alisema.
Kiongozi huyo akuwa Simba alionyesha ni
mwenye furaha kubwa kutokana safari hiyo ndefu kuwa na mafanikio.
Kutokana na kipigo hicho, Arsenal
imedondoka kutoka kileleni na kuipisha Chelsea iliyoibanjua Newcastle United
kwa mabao 3-0, yote yakipigwa na Eden Hazard.
0 COMMENTS:
Post a Comment