Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic,
amefunguka kuwa, anahofia kikosi chake kupata majeruhi katika kipindi hiki cha
lala salama kwani watamharibia mipango yake.
Simba ipo nafasi ya nne ya msimamo wa
ligi kuu kufuatia kuwa na pointi 30, nyuma ya Mbeya City yenye pointi 31,
ambapo inahitaji kujipanga ili iweze kufanikiwa kusonga mbele.
Loga
alisema anahofia majeruhi katika kikosi chake kwani wanaweza kusababisha
kutokuwa na kikosi kizuri kwa kuwa kila mchezaji anamtumia kulingana na mfumo.
“Ligi ni ngumu na hakuna timu kubwa wala ndogo
katika kipindi hiki kwani kila timu imejiandaa vya kutosha, hivyo tunahitaji
kujipanga pindi tunapokutana na timu yoyote.
“Kitu kikubwa kinachonipa hofu ni kuhusu
majeraha kwa wachezaji kwani yatasababisha kutokuwa na kikosi bora.
“Kwa sasa sina kikosi cha kwanza na
ninatumia mchezaji kulingana na mechi kwani kuna baadhi wanajua mfumo huu na
wengine wanajua mfumo mwingine, hivyo wote wapo sawa.
“Wachezaji ambao ni majeruhi kwa sasa ni
Said Nassoro ‘Chollo’ ambapo Donald Musoti alikuwa anasumbuliwa na malaria, pia
kuna baadhi ya wachezaji wanacheza huku wakisumbuliwa na majeraha
madogo-madogo,” alisema Loga.
0 COMMENTS:
Post a Comment