February 5, 2014



Kocha Msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwasa, alikuja juu baada ya mshambuliaji wa timu hiyo, Shabani Kondo, kufungwa pingu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Kondo alipigwa pingu Jumapili kufuatia kukaidi maagizo ya askari waliokuwa wakilinda usalama uwanjani hapo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga na Mbeya City.

Mkwasa alisema kuwa si sahihi kitendo walichokifanya polisi kwa kumfunga pingu mchezaji huyo na walichotakiwa kufanya ni kumweka chini ya ulinzi na kumuelewesha kosa lake.
“Ni kweli amefanya makosa lakini si sahihi kumfunga pingu kwani inamdhalilisha mchezaji husika ambapo polisi walitakiwa kumweka chini ya ulinzi na kumhoji na si kama walivyofanya,” alisema Mkwasa ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic