Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi,
amefunguka kuwa wanasahau kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Yanga, lakini
hawatapoteza pointi dhidi ya Simba na Mtibwa Sugar.
Mbeya City inatarajiwa kucheza na Simba
na Mtibwa kati ya tarehe 9 na 15 katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, uwanja
ambao wamekuwa wakipata matokeo mazuri.
Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Simba
kwenye Uwanja wa Taifa, vijana hao walifanikiwa kupata sare ya mabao 2-2.
Mwambusi
amesema wanasahau kipigo hicho, badala yake wanajiandaa dhidi ya Mtibwa ambayo
watakutana nayo wikiendi ijayo na baadaye watawasubiri Simba.
“Kitu kikubwa kilichotufanya tufungwe na
Yanga ni kutokana na mwamuzi kuwavuruga wachezaji wangu kisaikolojia.
“Kitendo cha kumpa mchezaji wetu muhimu
kadi nyekundu kilivuruga kabisa timu yangu baada ya kutulazimisha kubadili
mfumo mzima.
“Tunajiandaa kuweza kushinda katika uwanja wa
nyumbani ambapo nitatumia muda huu wa wiki moja kuweza kukiimarisha kikosi changu
ili tuweze kusonga mbele.
“Tunaamini kuwa Mtibwa Sugar na Simba
ambazo zinakuja kwetu hazitatoka na pointi.
“Baada ya mechi nne mbele ndiyo nitajua
nafasi ya timu yangu itakuwa wapi ukiachana na hii ya Yanga ambayo tumekutana
nayo leo,” alisema Mwambusi.
0 COMMENTS:
Post a Comment