Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic
amesema kuitoa Simba kwenye mbio za ubingwa msimu huu ni kosa kubwa.
Logarusic amesema Simba bado ina nafasi
ya kufanya vizuri kwa kuwa ligi bado mbichi na si kama wengi wanavyoamini.
“Sare yetu na Mbeya City haiwezi kuwa
imetutoa kwenye kuwania ubingwa. Bado tunapambana na tunataka kufanya vizuri,”
alisema.
Logarusic alisema Simba ni kati ya timu
zenye kikosi kizuri na chenye wachezaji wenye uwezo hivyo hawana sababu ya
kuhofia.
“Ushindani kwenye ligi leo unaiangusha
Simba, kesho timu nyingine. Lakini sisi bado hatujateteleka hata kidogo,”
alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment