Kocha Mkuu wa Azam FC, Mcameroon, Joseph
Omog, amesema kikosi chake kipo kamili kwa ajili ya michuano ya Kombe la
Shirikisho.
Azam itaingia kwenye Uwanja wa Chamazi
jijini Dar es Salaam keshokutwa Jumapili kuvaana na Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika
mchezo wa awali.
Kocha
huyo alisema kuwa katika michezo ya ligi kuu, amepata changamoto nyingi sana
ambazo zinampa nafasi ya kuweza kuendelea kukiboresha kiwango cha timu yake.
Alisema kwa sasa anaendelea kuangalia
kikosi chake kupitia ule upungufu alioweza kuubaini kwa ajili ya maandalizi ya
mchezo wao wa Jumapili.
“Nimepata matumaini makubwa sana kupitia
mechi za ligi kuu katika viwango vya wachezaji wangu, hasa kuelekea michuano ya
Kombe la Shirikisho tunayojiandaa nayo kwa sasa, japo muda umebaki mchache
sana.
“Naamini wapinzani wetu wa huko Msumbuji
ni wazuri japo siwafahamu na sijawahi
kuwaona lakini timu yangu bado naamini itafanya vyema kwa jinsi watakavyofuata kile ninachokifundisha na wakakielewa,” alisema
Omog.
Azam imepata nafasi hii baada ya kushika
nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment