Mechi ya kesho dhidi ya Mgambo JKT
inaumiza kichwa cha Kocha Zdravko Logarusic.
Kocha huyo raia wa Croatia anasema
sare dhidi ya Mtibwa imefanya aamini mechi za mikoani zitakuwa ngumu.
“Mazingira ni tofauti sana na Dar es
Salaam, viwanja na kila kitu. Lakini ni lazima kufanya kila linalowezekana ili
kushinda.
“Nimeambiwa mzunguko wa kwanza
tuliifunga timu hii mabao sita, lakini sasa imebadilika, utaona ilivyoanza
mzunguko wa pili.
“Maana yake ni mechi ya kisasi safari
hii wao wakiwa nyumbani. Hatuna ujanja, kwetu pointi tatu ni muhimu na
tunafanya kazi kwa nguvu sana,” alisema Logarusic.
Chini yake, Simba ilianza mzunguko wa
pili na ushindi mara mbili mfululizo, lakini ilipotoka nje ya Dar es Salaam,
mechi ya kwanza ilikuwa sare ya 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar mjini Morogoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment