Mshambuliaji wa Mtibwa
Sugar, Mussa Hassan Mgosi amesema kuwa timu yake ya zamani ya Simba ina wakati
mgumu iwapo inataka kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, msimu huu.
Baada ya mchezo baina ya timu hizo juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Mgosi alisema Simba ilionyesha kiwango cha chini hali ambayo amedai itawawia vigumu kupata matokeo mazuri katika michezo ijayo iwapo hawatabadilika.
“Simba wana wakati mgumu
sana wa kutwaa ubingwa kwa kiwango walichoonyesha katika mchezo huu,” alisema
Mgosi ambaye alifunga bao katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya 1-1.
Naye kiungo mshambuliaji
wa Mtibwa, Shaban Kisiga, alisema mechi hiyo ilikuwa ngumu lakini anashukuru
wameweza kupata pointi moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment