Na Lucy Mgina wa CHAMPIONI
MSHAMBULIAJI wa Yanga,
Jerry Tegete, ameamua kuokoka rasmi na kumrudia Mungu.
Jerry aliandika maneno
hayo kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Facebook, kuwa ameamua
kuokoka rasmi na kuachana na mambo ya kidunia kutokana na kushuhudia mama yake
mzazi ambaye anaumwa, akipata nafuu baada ya kuombewa na mchungaji.
Katika ukurasa wake huo,
Tegete aliandika: “Nipo Mwanza, nimekuja kumuona mama yangu anaumwa sana,
lakini kaja mchungaji kumuombea na mama kapata nafuu kabisa.
“Mungu ni mkubwa sana na
maisha ukimkabidhi Mungu kila kitu kinawezekana, maisha ya kidunia hayana maana
bila Yesu, nimeokoka rasmi.”
Baada ya kutuma ujumbe
huo, alipata wachangiaji zaidi ya 200 walioonekana kumuunga mkono na kumpongeza,
huku wakimpa pole kwa kumuuguza mama yake, alipopigiwa simu ilikuwa ikiita tu
bila kupokelewa kwa kuwa tayari alikuwa amesharejea Dar.
Alipopigiwa baba mzazi wa
Jerry, mzee John Tegete, alisema: “Ni kweli Jerry alikuwa hapa, lakini kaondoka
jana (juzi), alikuja kumuona mama yake ambaye amefanyiwa upasuaji wa goita na
sasa anaendelea vizuri. Hajaniambia habari za kuokoka, lakini kama ni hivyo
nampongeza.”
0 COMMENTS:
Post a Comment