MGOSI WAKATI AKIKIPIGA SIMBA |
Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mussa
Hassan Mgossi, anataka kuiadhibu timu yake ya zamani, Simba kwa kuhakikisha
Mtibwa inachukua pointi tatu keshokutwa Jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu Bara
kati yao kwenye Uwanja wa Jamhuri, Moro.
Mgosi aliichezea Simba kwa mafanikio
makubwa na alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2009/2010 wakati
Wekundu wakitwaa ubingwa. Keshokutwa ataivaa timu yake hiyo ya zamani akitaka
pointi tatu muhimu.
Mgosi amesema ligi ni ngumu nakwa upande
wao, baada ya kufungwa na Azam na kutoka suluhu na Kagera, wanataka kuonja
ushindi wa kwanza wa mzunguko wa pili dhidi ya Simba.
“Ligi ni ngumu, kuna ushindani wa hali ya juu
na tunahitaji kushinda mchezo wetu, nimejiandaa vyema ili kuweza kufunga katika
mchezo huo, lengo letu ni kuhakikisha tunaisaidia timu yetu ili iweze
kufanikiwa kumaliza katika nafasi nzuri,” alisema Mgosi.
0 COMMENTS:
Post a Comment