UKIANGALIA karibu kila mechi anayocheza
kiungo Jonas Mkude wa Simba, utagundua anaonyesha uwezo wa juu sana.
Moja ya matatizo makubwa ya timu nyingi
ninamba sita, yaani kiungo mkabaji au hub kama Waingereza wanavyosema.
Pamoja na kuwa na umri wa kati, Mkude
amekuwa akionyesha uwezo mkubwa kiuchezaji, kukaba, kutoa pasi za uhakika
zikiwemo pasi zao, yaani za zinazozaa mabao.
Ukiachana na yote hayo, Mkude amekuwa
akifunga mara kadhaa, tena anafunga mabao ya kiwango cha juu kabisa yanayoweza
kuwania nafasi ya bao bora la Ligi Kuu Bara na kushinda.
Lakini ukiangalia katika mwenendo wa
uchezaji, anakosa mwendelezo, si mtu anayeweza kucheza mechi nne au tano.
Atacheza moja, inayofuata atajitahidi
baada ya hapo ni benchi na anaweza kujikuta kwenye matatizo na kocha au lolote
lile.
Uhakika ni hivi, Mkude hana consistence
(muendelezo) katika uchezaji wake, kitu ambacho si kizuri kwake.
Inawezekana hajitambui, kwamba kwa umbo
lake, nguvu, uwezo wa kucheza ingekuwa vizuri wakati huu angekuwa ameondoka
Simba.
Lazima awe na muhu ya mafanikio, lakini
waliomzunguka wakiwemo makocha na watu wenye nia nzuri wamueleze ukweli badala
ya kumuonea haya.
Kwamba ana uwezo mzuri, mkubwa na
unaweza kukua na kuwa mkubwa zaidi kama atataka kufanikiwa zaidi, lakini si kwa
mwendo anaokwenda nao.
Mkude ni aina ya viungo ambao Tanzania inawahitaji,
kuanzia kwenye timu au hata timu ya taifa na wanaweza kuwa msaada mkubwa.
Lakini ni kati ya viungo wanaohitajika
kuipa sifa Tanzania ya kuwa na wachezaji wa kulipwa wanaofanya vizuri ili
kuwavutia watu wa Ulaya, Asia na kwingineko kutafuta Watanzania zaidi.
Yote yanawezekana kwa Mkude lakini kwa
mwendo anaokwenda nao sasa, hatafika mbali. Muelezeni ukweli, akikasirika
lakini mwisho ataelewa tu!
0 COMMENTS:
Post a Comment