Kamati ya rufaa ya Shirikisho la Soka
la Hispania, limeamua kuacha adhabu ya kutocheza mechi tatu kwa mshambuliaji
Cristano Ronaldo wa Real Madrid iendelee.
Kamati hiyo imeona Madrid haikuwa na
sababu ya kukata rufaa baada ya Ronaldo
kukumbana na kifungo hicho.
Ronaldo alihkumiwa baada ya kumpiga
kichwa na kuzua tafrani katika mechi dhidi ya Athletic Bilbao.
Kutokana na uamuzi huo, maana yake
Ronaldo atakosa mechi dhidi ta Villareal itakayopigwa Jumamosi ingawa taarifa
zimeeleza, Gareth Bale aliyekuwa majeruhi atarejea.
Ronaldo pia anatuhumiwa kumuonyesha
ishara isiyo sahihi kimichezo mwamuzi wa akiba wakati akitoka baada ya kulambwa
kati hiyo ya njano.
Mwamuzi aliyechezesha mechi hiyo pia
amelambwa adhabu ya kufungiwa pamoja na kutochezesha mechi za Madrid kwa msimu
huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment