Timu ya soka ya Mtibwa Sugar imesema
imejipanga kikamilifu kuikabili Simba na kwamba wasitegemee ushindi.
Simba inavaana na Mtibwa leo, Jumatano kwenye
Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro katika mchezo mkali wa Ligi Kuu ya Tanzania
Bara.
Meneja wa timu hiyo, David Gboya,
alisema timu ya Simba ni nzuri lakini hata wao wana timu nzuri na mwisho wa
siku wanategemea ushindi.
"Siyo kwamba tunacheza na Simba
ndiyo twende kinyonge bali tunaenda kupambana ili tuibuke na ushindi
ukizingatia tumepoteza mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Azam na wa pili tumetoka
sare dhidi ya Kagera.
“Tunaamini kuwa tuna uwezo wa hali ya
juu wa kuibuka na ushindi kwa kuwa tumejiandaa vyema na hatuna hofu yoyote hadi
sasa,” alisema Gboya.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa
kusisimua na Simba wanafahamu kuwa ushindi tu ndiyo utafufua matumaini yao ya
kutwaa ubingwa msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment