Mtibwa Sugar imeipunguza kasi Simba baada ya
kutoka nayo sare ya bao 1-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja Jamhuri
mjini Morogoro.
Mechi hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu,
ilikuwa ni ya Mtibwa Sugar katika kipindi cha kwanza ambayo ilianza kupata bao
kupitia kwa Mussa Hassan Mgosi.
Mgosi, mshambuliaji wa zamani wa Simba alifunga
bao hilo baada ya kuiwahi krosi iliyochongwa safi na kupiga kichwa kilichomzidi
Ivo Mapunda.
Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha pili, Simba iliposawasiaha
kupitia Mrundi, Amissi Tambwe aliyefunga bao lake la 14 katika ligi hiyo.
Baadaye kiungo mkongwe wa Mtibw Sugar, Shabani
Nditi alilambwa kadi nyekundu kwa madai alimtolea lugha chafu mwamuzi Donisya
Nkurya wa Arusha.
Kabla ya mechi hiyo, Simba iliiadhibu JKT Oljoro
kwa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, kabla ilikuwa imeichapa Rhino
ya Tabora, bao -10 kwenye uwanja huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment