Mashabiki wa Simba waliokuwa wamekwenda
mjini Mbeya kuishangilia timu yao katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya
City, wamelalama.
Wakizungumza na blog hii, mashabiki hao
wamesema Mbeya City walifanya vitendo vingi vya kuiungwana ikiwa ni pamoja na
kumchania jezi shabiki mmoja wa Simba.
“Hata sisi Simba na Yanga, kuna ugomvi
uwanjani tu hasa shabiki anapokwenda kukaa upande ambao si sahihi.
“Lakini Mbeya City walikuwa wakifanya
unyama huo mitaani, walimrukia na kumchania jezi mwanachama wa Simba.
“Sasa timu gani inataka kucheza bila ya
wapinzani, tatizo ni lipi mtu kuvaa jezi yake. Kweli hawakuwa sahihi,” alisema
Ngade.
“Nafikiri kuna kila sababu walifanyie
kazi hilo, maana walipokuja hapa Dar utaona hakuna mtu aliyewafanyia vurugu.”
Katika mechi hiyo, Simba na Mbeya City
zilimaliza mchezo kwa sare ya bao 1-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment