YANGA inashuka dimbani leo katika mechi
yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuwavaa vibonde Komorozine de Moroni
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Wiki mbili baadaye Yanga itakuwa Moroni
kurudiana na mabingwa hao wa Comoro, lakini muhimu zaidi ni mechi ya leo Taifa.
Timu huyo inajulikana kuwa ni kibonde
kutokana na historia ya soka katika nchi hiyo.
Hata Yanga imewahi kuanza michuano hiyo
na timu kutoka Comoro na ‘kujipigia’ inavyotaka.
Hali hiyo imejenga dharau hata kwa
mashabiki kwamba Yanga ina kazi lahisi sana leo, kitu ambacho si sahihi.
Mashabiki wanaweza kufikiri hivyo,
lakini litakuwa kosa kubwa kwa wachezaji wa Yanga kuingia huko, watakwisha.
Wanachotakiwa ni kuifunga timu hiyo hata
mabao 20 kama itawezekana.
Lakini kuwa makini kwa kuwa ni timu ya
mpira ambayo uwezo wake haujaonekana, hakuna anayejua, hivyo lazima wacheze kwa
umakini mkubwa.
Yanga haitaungwa mkono na Wanayanga
pekee kwa mechi ya leo, badala yake Watanzania waelewa na wazalendo kwa ajili
ya nchi.
Hivyo uwakilishi wa Yanga kwa leo
utakuwa mkubwa zaidi na lazima watambue kwamba hakuna utani.
Ushindi utakaopatikana kama ni mkubwa ni
bora zaidi pia uwe sehemu ya kuwafanya Al Ahly waingie hofu hata kama Yanga
haikucheza na timu kibonde.
Kuwaza mmevuka kabla ya kuingia uwanjani
ni kosa na kuna mifano mingi ambayo imewahi kutoa, ninaamini wachezaji wa Yanga
watakuwa wanaikumbu. Hivyo wajifunze kupitia mifano hiyo ili kufanya vizuri
leo.
KILA LA KHERI YANGA, KILA LA KHERI
TANZANIA.
0 COMMENTS:
Post a Comment