Baada ya
timu ya soka ya Ndanda ya mkoani Mtwara kufanikiwa kupanda daraja hadi LIgi Kuu
Bara, sasa wachezaji wa timu hiyo wataondoka Dar es Salaan keshokutwa Ijumaa na
kurudi mkoani humo kwa usafiri wa ndege wa Shirika la Tanzania (ATC).
Hiyo
itakuwa ni mara ya kwanza kwa wachezaji wa Ndanda kusafari kwa ndege tangu
ilipoanzishwa Mach 28, 2011 katika kijiji cha Ndanda kilichopo wilayani Masasi.
Katibu Mkuu
wa Ndanda, Selemani Kachele aliliambia Championi Jumatano kuwa baada mkuu wa
mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia, kupata taarifa za timu hiyo kupanda daraja
aliamua kutoa ofa hiyo kwa wachezaji pamoja na viongozi wote wa kikosi hicho.
Alisema
kuwa, Simbakalia amefanya hivyo kama moja ya shukrani zake kwa wachezaji pamoja
na viongozi kwa jitihada zao walizozionyesha kwenye michuano hiyo ya Ligi Daraja
la Kwanza na kufanikiwa kupanda daraja mpaka Ligi Kuu Bara.
“Mbali na
hilo pia ametuandalia sherehe kubwa ambayo itaambatana na mapokezi ya aina yake
mara tu tutakapotua mjini Mtwara siku hiyo ya Ijumaa.
“Hakika tunamshukuru
kwa mchango wake huo na tunawaomba wananchi wa Mtwara kujitokeza kwa wingi siku
hiyo kwa lengo la kuwapokea vijana wao waliopigana kwa nguvu zote na kurudisha
heshima ya mkoa wetu iliyokuwa imepotea kwa miaka 10 tangu Bandari iliposhuka
daraja,” alisema Kachele .
0 COMMENTS:
Post a Comment