Mshambuliaji nyota wa Yanga, Emmanuel Okwi amesema kila inapofika usiku amekuwa akitumia
muda wake kutafakari kuhusiana na mabao.
Ameiambia
SALEHJEMBE kwamba, mara kadhaa kila
anapokuwa
ametulia usiku amekuwa akijiuliza namna ya kufanya kuhakikisha anafunga katika
mechi ya leo dhidi ya Prisons ya Mbeya.
“Hata kama
nikishindwa kufunga, basi angalau nitoe hata pasi tatu za mabao. Natamani
tuendelee kushinda kama ilivyokuwa Tabora.
“Lakini pia
ninataka kufunga, kwa mchezaji kufunga bao kwa ajili ya timu yako ni jambo jema
sana. Lakini sisemi ni lazima, kama ikiwa ni sehemu ya kutoa pasi, nitafanya
hivyo mara moja,” alisema Okwi.
Mganda huyo
aliyewahi kukipiga Simba, amekaukiwa mabao baada ya kuichezea Yanga mechi tano na
kufunga bao moja tu.
Lakini
amekuwa chachu ya pasi za mabao ya Yanga na pia msumbufu kwa mabeki wa timu
pinzani.
Okwi
anasifika kwa kasi na chenga za maudhi, lakini akipata nafasi amekuwa akifunga
kwa mashuti makali.
Okwi
amewahi kukipiga Simba na kujenga jina kubwa nchini kabla ya kuondoka na kwenda
kujiunga na Etoile du Sahel ya Tunisia.
0 COMMENTS:
Post a Comment