Kiungo wa Coastal Union, Haruna Moshi
‘Boban’, huenda asiongeze mkataba katika
kikosi chake hicho.
Boban alitua Coastal Union msimu huu
mwanzoni baada ya kumaliza mkataba wake na Simba msimu uliopita na kufanikiwa
kupewa mkataba wa mwaka mmoja ambao unakaribia kumalizika.
Chanzo cha karibu cha mchezaji huyo,
kilisema kuwa kiungo huyo kwa sasa hana mpango wa kuongeza mkataba ili
kuendelea kuitumikia timu hiyo kutokana na baadhi ya mambo ambayo yanaendelea
katika timu hiyo, japo hajataka kuyaweka wazi.
Aidha, chanzo hicho kilisema kuwa,
dalili zinaonyesha wazi kabisa kwamba hatarudi tena kwenye kikosi hicho baada
ya mkataba kumalizika.
“Ni kweli yule Boban ni rafiki yangu lakini ni
wazi kwamba hana mpango wa kuongeza mkataba tena ili kuendelea kuwa katika timu
hii msimu ujao, lakini hataki kuweka wazi sababu zipi zinamfanya ashindwe
kuongeza mkataba hapo klabuni,” kilisema chanzo.
0 COMMENTS:
Post a Comment