Kocha Mkuu
wa Simba, Zdravko Logarusic, amemtimua kipa wa timu hiyo, Abuu Hashim, baada ya
kukwaruzana naye kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja
wa Kinesi uliopo Ubungo, Shekilango jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika uwanjani hapo juzi (Jumatatu), kocha
wa makipa wa timu hiyo, Iddi Pazi 'Father', alisema kipa wake huyo hayupo
uwanjani baada ya kutimuliwa na kocha mkuu wa kikosi hicho (Loga).
“Leo ndiyo
tumeanza mazoezi baada ya kumaliza mapumziko mafupi lakini kipa wangu, Abuu
Hashim, ametimuliwa na kocha mkuu baada ya kuhitilafiana kwenye mazoezi
yaliyofanyika siku ya mwisho.
Baada ya
kutibuana naye, alimpiga marufuku kukanyaga mazoezini mpaka atakapomuita, sasa
sijui atamuita lini,” alisema Father.
Kocha huyo
wa makipa alisema chanzo kikubwa cha kutimuliwa kipa huyo ni kushindwa kufuata
maagizo ya Loga kwenye mazoezi na alipomuuliza alimwambia hajisikii vizuri,
anaumwa ndipo Loga akamuona kama muongo akaanza kumbwatukia na kumtimua.
Akizungumzia
tukio hilo, Loga amesema ameamua kumpumzisha kipa huyo kwa muda mpaka
atakapojisikia nafuu na kukataa kulizungumzia kiundani sakata hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment