MZEE AKILIMALI (KATIKATI) |
Bodi ya Udhamini ya Yanga, imezuia
maandamano ya wanachama na wapenzi wa wa klabu hiyo, yaliyokuwa yafanyike kesho
Jumanne hadi Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete iwapo Manispaa ya Ilala haitatoa
kibali cha ujenzi wa uwanja wao wa kisasa.
Awali kupitia kiongozi wa wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali walitaka kuandamana kutokana na
ukimya wa Manispaa ya Ilala, licha ya kuwasilisha barua tangu mwaka jana
wakiomba kuongezewa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kisasa Jangwani.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Yanga,
Benno Njovu, katika kikao cha bodi ya wadhamini kilichochukua saa tatu jana, wajumbe
waliamua kusitisha maandamano hayo na kuwaomba wanachama kusubiri hadi bodi
ikutane kwanza na uongozi wa manispaa chini ya Meya wa Jiji, Jerry Slaa kujua mustakabali
wa ombi lao.
Kikao hicho kilihudhuriwa na mwenyekiti
wa bodi hiyo, Kapteni George Mkuchika, wajumbe wengine ni mama Fatma Karume,
Francis Kifukwe, Jabir Katundu na Ammy Mkungwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment