KIKOSI CHA MBEYA CITY |
Uongozi wa Mbeya City ya jijini Mbeya,
unatarajia kuwasilisha barua ya malalamiko dhidi ya Rhino Rangers kwa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mbeya City haikufurahishwa na mchezo wa
kibabe uliochezwa na Rhino katika mchezo wa Ligi Kuu Bara baina ya timu hizo
Machi 8, mwaka huu, ingawa ilipata ushindi wa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa
Sokoine, Mbeya.
Timu hiyo inayokamata nafasi ya tatu
kwenye ligi hiyo, inalalamika Rhino waliambiwa na viongozi wao wacheze mchezo
mchafu, hali iliyosababisha kipa wao amvunje mbavu kiungo wao mshambuliaji,
Richard Peter.
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, amesema wameamua kuiandikia barua
TFF kulalamikia mchezo huo, pia wakimlalamikia mwamuzi kwamba hakuchezesha
katika kiwango kinachotakiwa.
“Tunatarajia kuandika barua kupeleka TFF
kumlalamikia msimamizi wa mechi pamoja na mwamuzi na kipa kwa jambo
walilolifanya, kwani licha ya tukio hilo kutokea lakini hakutoa adhabu yoyote
kwa kipa.
“Alianza kwa kumrukia Mwegane Yeya
lakini mwamuzi hakufanya kitu na baadaye akamrukia Peter na kumsababishia
matatizo kwa kumvunja mbavu, kwa jumla maamuzi ya mzunguko wa pili yanaonekana
siyo sahihi kwani yamelenga kutuharibia zaidi,” alisema Kimbe.
0 COMMENTS:
Post a Comment