Rapa maarufu Drake ‘ameshoo’ love kwa wachezaji wawili wa Ligi Kuu
England wakati alipokuwa katika ziara yake nchini humo.
Drake raia wa Canada alikutana na Daniel Sturridge wa Liverpool
pamoja na Samir Nasri wa Manchester City.
Walipata nafasi ya kufanya mazungumzo kidogo, kabla ya wachezaji
hao kumpa jezi zilizokuwa zina saini zao na wachezaji wengine.
Sturridge na Nasri wamekuwa mashabiki wakubwa wa Drake mwenye umri
wa miaka 27.
0 COMMENTS:
Post a Comment