Mshambuliaji wa Galatasaray ya Uturuki, akiwa na wenzake amefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Stamford Bridge unaotumiwa na Chelsea.
Mara tu baada ya mazoezi, Drogba amesema yuko tayari kwa ajili ya mechi ya leo dhidi ya kikosi hicho cha Jose Mourinho katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Nimerudi tena hapa, kwangu ni sehemu bora na yenye kumbukumbu nyingi sana. Lakini kama ni mechi, niko tayari," alisema Drogba.
Katika mechi ya kwanza jijini Istambul, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1. Hivyo jibu litatapikana leo.
0 COMMENTS:
Post a Comment