Dunia kweli ina mambo! Hebu sikiliza mpya hii imeibuka katika timu ya Lipuli ya Iringa inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, baada ya viongozi wake kulalamikiwa kuuza mechi za ligi na kutowalipa wachezaji wao mishahara kwa muda, sasa kuna kubwa kuliko zote, isome vizuri katika aya zinazofuata.
Wachezaji hao wameamua kufunguka kuwa baada ya kuona hali inazidi kuwa
mbaya katika kikosi hicho, kwa kusema kuwa kuna hatua imefika viongozi wao
wamekuwa wakiwaomba wachezaji fedha za kununua vocha.
“Ukweli timu yetu mambo si shwari, hakuna
kulipwa mishahara maisha tunayoishi ni ya kuungaunga, cha ajabu hata baadhi ya viongozi wenye
mambo magumu wanafikia hatua ya kuomba hela za vocha kwetu au hata kuazima simu
zetu.
“Ajabu kabisa ni kuwa wapo (viongozi) ambao wamediriki hata kuweza
kuuza mechi yetu dhidi ya Kimondo FC,” alisema mchezaji mmoja wa Lipuli,
mwingine akadakia kwa kusema kuwa wakihoji juu ya malipo yao wanaambiwa
waondoke klabuni.
Championi Jumamosi lilipomtafuta Mwenyekiti wa Lipuli, Abdu Changawa na kumsomea madai hayo,
alisema: “Tuhuma hizo si za kweli, ni baadhi tu ya watu wanaotaka
kutuchafua na nia yao ni kupata madaraka katika hii timu. Wachezaji wangekuwa
hawalipwi wangepata wapi hamasa ya kucheza na kufikisha pointi 20!”
0 COMMENTS:
Post a Comment