Kiungo wa Simba, Uhuru Selemani amesema amebakiza muda
mchache wa kuendelea kuitukia timu hiyo kwa kuwa tayari ameshapata dili la
kucheza soka la kulipwa nchini Ufaransa, pia hata klabu
yake hiyo imeonekana kumdharau.
Uhuru amesema kuwa kitu kinachomuondoa Simba ni kutothaminiwa
na pia anatumia muda mwingi kujitoa kwenye timu hiyo lakini fadhila zake ni
chache.
Alisema kuwa anatumia muda mwingi kufanya mazoezi lakini matokeo yake
nafasi ya kucheza uwanjani ni ndogo, kitu
ambacho kinamvunja moyo na kuonekana kama hana thamani, hivyo ni bora aondoke.
“Ungekuja mazoezini uone ninachofanya halafu siku ya mechi nacheza
muda mdogo sana lakini mashabiki wanatamani niwe nacheza kwa kipindi kirefu hii
inavunja moyo kuliko maelezo,” alisema Uhuru.
Aliongezea kuwa toka alipoichezea Simba, hajawahi kulalamika hivyo
wakiona mtu analalamika lazima wamsikilize. “Kitu ninachoshukuru muda wangu
umebaki mchache kuichezea Simba, nitaondoka kuangalia maslahi yangu huko na
wala sitatoroka,” alimalizia Uhuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment