KAPOMBE WAKATI AKIWA CANNES |
KochaMkuu wa Simba, Mcroatia Zdravko Logarusic, ameamua kutenga muda wake na kuingia
kwenye mtandano wa YouTube, maalum kwa ajili ya kumfuatilia Shomari Kapombe
ambaye anatajwa kuwa mbioni kurejea kikosini hapo.
Loga ameshapewa taarifa juu ya Kapombe ambaye bado ana mkataba na
Klabu ya AS Cannes ya Ufaransa, kuwa anaweza kujiunga na timu hiyo baada ya
kutokuwa na maelewano mzuri na klabu hiyo ya Ufaransa.
Loga amezungumza na SALEHJEMBE na kusema kuwa amefanya hivyo kwa kuwa
alihitaji kumfahamu mchezaji huyo, ili kuhakikisha anajua jinsi ya kumtumia pindi
atakapotua klabuni hapo.
“Niliomba jina lake ili nikamuangalie YouTube kwanza, nimemuona kwamba
ni mzuri lakini mpira upo tofauti na vitu vingine, huwezi jua kwa sasa ana
kiwango cha namna gani kwa muda wote aliokuwa nje.
“Mpira ni mchezo wa kuonekana unapokuwa uwanjani, nitajihakikishia
zaidi pale atakapotua kweli na kuanza mazoezi pamoja na wenzake ndiyo
nitagundua kuwa ana kiwango gani na nimtumie vipi kwenye kikosi changu,”
alisema Loga.
Kapombe aliondoka nchini na kujiunga na AS Cannes wakati huo Simba ikiwa chini ya Mfaransa, Patrick Liewig.
Hivyo hakupata nafasi ya kumuona akiitumikia Simba, tayari viongozi wa Simba wameanza juhudi za kutaka kumrejesha baada ya kufanya mazungumzo ya awali na AS Cannes.
Lakini Azam FC na Yanga wamekuwa wakimuwania na kuna taarifa wamekuwa wakifanya naye mazungumzo na AS Cannes ilishaonya.
Pia kuna taarifa, Azam FC imekuwa ikimshawishi kuvunja mkataba ili impate kwa ulaini.
0 COMMENTS:
Post a Comment