Kocha Mkuu wa Simba, Mcroatia, Zdravko
Logarusic, amelitaja suala la kutokuwa na uamuzi wa haraka ni moja ya tatizo kubwa kwa wachezaji wake.
Mcrotia huyo ambaye ameanza kuinoa timu
hiyo katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara na timu imekuwa haina matokeo mazuri.
Awali, wachezaji wake walidai kwamba
tatizo kubwa ni ukali wake, lakini mwenyewe ameamua kuwarudishia lawama kwa
kusema wana akili nzito katika kufanya maamuzi.
Loga
alisema kikosi hicho kina wachezaji wengi wazuri lakini bado wengi wao
hawatambui kitu gani wanatakiwa kufanya ili waweze kuisaidia timu yao kufanya
vyema, hasa katika upigaji wao pasi ambao bado si mzuri.
“Wachezaji
wangu ni wazuri na wanaweza kubadilika na kuwa na ‘performance’ nzuri lakini
tatizo lao bado hawana ule uamuzi wa haraka katika kufanya mashambulizi, pale mchezaji
anapopata mpira.
“Na hata upigaji wao wa pasi bado siyo mzuri,
wanapiga pasi fupi, wanatakiwa wafahamu kusoma hata mawazo za wapinzani siyo
unapiga tu ilimradi. Lazima uwe umelenga kuwa kitu fulani chaweza kutokea na
wajielewe nini wanatakiwa kufanya wawapo uwanjani,” alisema Logarusic.
0 COMMENTS:
Post a Comment